Top40-Charts.com
Support our efforts,
sign up for our $5 membership!
(Start for free)
Register or login with just your e-mail address
 Videos 

TOTO AFRICANS 0-3 YANGA SC: HIGHLIGHTS (MECHI YA KIRAFIKI - 10/09/2019)

Timu ya Wananchi, Yanga SC leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Magoli ya Yanga yamefungwa na David Molinga aliyefunga mawili dakika ya 36 na 40 huku la tatu likifungwa na Abdul-aziz Makame dakika ya 48. Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya kambi ya Yanga jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia utakaopigwa kwenye Uwanja wa taifa Septemba 14 mwaka huu. Katika mchezo wa kwanza wa kirafiki, Yanga ilicheza na Pamba SC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Top songs from around the world today


© 2001-2025
top40-charts.com (S6)
about | site map
contact | privacy
Page gen. in 0.2638049 secs // 54 () queries in 0.021303415298462 secs