Timu ya Wananchi, Yanga SC leo imeng’ang’aniwa na KMC ikilazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia, Yanga wametangulia kupata bao kupitia kwa Mrisho Ngasa dakika ya 73, lakini KMC wakasawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 90+4 kupitia kwa Abdul Hillary baada ya Hassan Kabunda kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Matokeo hayo yanaifanya ifike nafasi ya 9 ikiwa imefikisha pointi 17 katika mechi 8 ambazo imecheza.